Saturday, 4 June 2016



NENO KUTOKA KWA MKUU WA SHULE


Natumia fursa hii kumshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kutulinda na kutufikisha muda huu. Pia natumia muda huu kutoa shukurani zetu za dhati kwa  wizara ya eilmu, sayansi, teknolojia, elimu ya juu na ufundi, Mhe. Mbunge, Mhe.  Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Mhe.Mkurugenzi wa halmashauri, waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara, walimu, wazazi, wadau wa elimu na wanafunzi kwa ujumla kwa ushiriakiano wanaouonesha katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika tasinia ya elimu.
Shule ya sekondari Nyakahura ilianza mwaka 2002 ikiwa ni ya kutwa tu. Kwa sasa shule yetu ni ya kutwa na bweni, Kidato cha kwanza hadi cha nne ni kutwa na Kidato cha tano  na sita ni bweni. Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi iliipa hadhi shule ya kuwa elimu ya juu ya sekondari mwaka 2010. Shule inajumla ya wanafunzi 879, wavulana wakiwa 496 na wasichana 383.  Shule ina wafanyakazi 45, kati yao, wapishi ni 03, walinzi 03, Karani  01, walimu wa sayansi wa muda  04 , na walimu walioajiriwa na serikali 34.
Kitaaluma, shule yetu imekuwa mstari wa mbele katika kudumisha taaluma kiwilaya, kimkoa, na kitaifa na kupata mafanikio makubwa ya kidato cha pili, cha nne na cha  sita. Ufuatao ni mwainisho wa matokeo ya kidato cha pili, cha nne na sita kwa mwaka  kuanzia mwaka 2013 hadi 2015
Kidato cha Pili
2013
2014
2015
A – 03
B – 42
C – 19
D – 00
F – 00
Ufaulu 100%
Distinction  - 16
Merit  - 20
Credit – 28
Pass – 08
Fail – 00
Ufaulu 100%
Distinction  - 07
Merit  - 27
Credit – 31
Pass – 17
Fail – 00
Ufaulu 100%

Kidato cha Nne
2013
2014
2015
Daraja I – 00
Daraja la II – 05
Daraja la III – 05
Daraja la IV – 31
Daraja la 0 – 15 
Ufaulu 77%
Distinction  - 00
Merit  - 08
Credit – 10
Pass – 15
Fail – 09
Ufaulu 79%
Daraja I – 00
Daraja la II – 04
Daraja la III – 14
Daraja la IV – 37
Daraja la 0 – 04
Ufaulu 93%



Kidato cha Sita
2012/2013
Mwaka 2013/ 2014
Mwaka 2014 /2015
Daraja I – 00
Daraja la II – 15
Daraja la III – 42
Daraja la IV – 00
Daraja la 0 – 00
Ufaulu 100%
Daraja I – 09
Daraja la II – 37
Daraja la III – 17
Daraja la IV – 00
Daraja la 0 – 00 
Ufaulu 100%
Distinction  - 24
Merit  - 44
Credit – 07
Pass – 00
Fail – 00
Ufaulu 100%




 Kimichezo. Shule yetu inafanya vizuri katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu ,mpira wa mikono na wavu. Hii imepelekea wanafunzi wetu kushiriki mashindano mbalimbali ya UMISETA kikanda na kitaifa.
Kimazingira. Kama sera ya kitaifa na Kimataifa inavyoelekeza kutunza mazingira, nasi pia Nyakahura sekondari hatuko nyuma, tumeanzisha bustani mbalimbali za miti, maua na kuboresha usafi wa mazingira kila siku.
Vilevile Shule yetu ina klabu mbalimbali mfano klabu ya kupambana na kuzuia rushwa (PCCB), klabu ya mali hai (environmental club), klabu ya wanafunzi yatima (NYOA) na klabu ya FEMA, ambazo zinatoa elimu kwa wanafunzi kuhusu mambo mbalimbali.
Tunaishukuru serikali kwa ujumla kwa kutupatia mradi wa maji kwani kwa sasa Jumuiya nzima ya wananyakahura sekondari hatuna tatizo la maji kwa wanafunzi pamoja na wafanyakazi wote.
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wadau wote wa elimu waliochangia kwa namna moja au nyingine kuhakikisha kuwa shule tunasonga mbele kitaaluma. Aidha nitoe rai kwao kuendelea kuchangia maendeleo ya elimu katika taasisi yetu kwani elimu ndio mkombozi wetu wa leo na kesho. Mungu ibariki Nyakahura sekondari, Mungu ibariki Tanzania.
Ahsanteni
Mwl.Regius K.Ishengoma
MKUU WA SHULE
MOTTO WETU: ELIMU NI UKOMBOZI.


1 comment: