NENO KUTOKA KWA MKUU WA SHULE
Natumia
fursa hii kumshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kutulinda na
kutufikisha muda huu. Pia natumia muda huu kutoa shukurani zetu za dhati kwa wizara ya eilmu, sayansi, teknolojia, elimu ya
juu na ufundi, Mhe. Mbunge, Mhe. Mkuu wa
Wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Mhe.Mkurugenzi wa
halmashauri, waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara, walimu, wazazi, wadau wa
elimu na wanafunzi kwa ujumla kwa ushiriakiano wanaouonesha katika kusukuma
gurudumu la maendeleo katika tasinia ya elimu.
Shule
ya sekondari Nyakahura ilianza mwaka 2002 ikiwa ni ya kutwa tu. Kwa sasa shule
yetu ni ya kutwa na bweni, Kidato cha kwanza hadi cha nne ni kutwa na Kidato
cha tano na sita ni bweni. Wizara ya
elimu na mafunzo ya ufundi iliipa hadhi shule ya kuwa elimu ya juu ya sekondari
mwaka 2010. Shule inajumla ya wanafunzi 879, wavulana wakiwa 496 na wasichana
383. Shule ina wafanyakazi 45, kati yao,
wapishi ni 03, walinzi 03, Karani 01,
walimu wa sayansi wa muda 04 , na walimu
walioajiriwa na serikali 34.
Kitaaluma,
shule yetu imekuwa mstari wa mbele katika kudumisha taaluma kiwilaya, kimkoa,
na kitaifa na kupata mafanikio makubwa ya kidato cha pili, cha nne na cha sita. Ufuatao ni mwainisho wa matokeo ya
kidato cha pili, cha nne na sita kwa mwaka
kuanzia mwaka 2013 hadi 2015
Kidato cha Pili
2013
|
2014
|
2015
|
A – 03
B – 42
C – 19
D – 00
F – 00
Ufaulu 100%
|
Distinction - 16
Merit - 20
Credit – 28
Pass – 08
Fail – 00
Ufaulu 100%
|
Distinction - 07
Merit - 27
Credit – 31
Pass – 17
Fail – 00
Ufaulu 100%
|
Kidato cha Nne
2013
|
2014
|
2015
|
Daraja I – 00
Daraja la II – 05
Daraja la III – 05
Daraja la IV – 31
Daraja la 0 – 15
Ufaulu 77%
|
Distinction - 00
Merit
- 08
Credit – 10
Pass – 15
Fail – 09
Ufaulu 79%
|
Daraja I – 00
Daraja la II – 04
Daraja la III – 14
Daraja la IV – 37
Daraja la 0 – 04
Ufaulu 93%
|
Kidato cha Sita
2012/2013
|
Mwaka
2013/ 2014
|
Mwaka
2014 /2015
|
Daraja I – 00
Daraja la II – 15
Daraja la III – 42
Daraja la IV – 00
Daraja la 0 – 00
Ufaulu 100%
|
Daraja I – 09
Daraja la II – 37
Daraja la III – 17
Daraja la IV – 00
Daraja la 0 – 00
Ufaulu 100%
|
Distinction - 24
Merit
- 44
Credit – 07
Pass – 00
Fail – 00
Ufaulu 100%
|
Kimichezo. Shule yetu
inafanya vizuri katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu ,mpira wa
mikono na wavu. Hii imepelekea wanafunzi wetu kushiriki mashindano mbalimbali
ya UMISETA kikanda na kitaifa.
Kimazingira. Kama
sera ya kitaifa na Kimataifa inavyoelekeza kutunza mazingira, nasi pia Nyakahura
sekondari hatuko nyuma, tumeanzisha bustani mbalimbali za miti, maua na
kuboresha usafi wa mazingira kila siku.
Vilevile
Shule yetu ina klabu mbalimbali mfano klabu ya kupambana na kuzuia rushwa
(PCCB), klabu ya mali hai (environmental club), klabu ya wanafunzi yatima
(NYOA) na klabu ya FEMA, ambazo zinatoa elimu kwa wanafunzi kuhusu mambo
mbalimbali.
Tunaishukuru
serikali kwa ujumla kwa kutupatia mradi wa maji kwani kwa sasa Jumuiya nzima ya
wananyakahura sekondari hatuna tatizo la maji kwa wanafunzi pamoja na wafanyakazi
wote.
Mwisho
kabisa napenda kuwashukuru wadau wote wa elimu waliochangia kwa namna moja au
nyingine kuhakikisha kuwa shule tunasonga mbele kitaaluma. Aidha nitoe rai kwao
kuendelea kuchangia maendeleo ya elimu katika taasisi yetu kwani elimu ndio mkombozi
wetu wa leo na kesho. Mungu ibariki Nyakahura sekondari, Mungu ibariki
Tanzania.
Ahsanteni
Mwl.Regius
K.Ishengoma
MKUU
WA SHULE
MOTTO WETU: ELIMU NI UKOMBOZI.