Tuesday, 28 June 2016

JOINING INSTRUCTION 2016



                                     JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                             WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI
 HALMASHAUI YA WILAYA  YA BIHARAMULO

                                                                                                                                      SHULE  YA SEKONDARI NYAKAHURA,
                                                                                                                                                            S.L.P.193, 
                                                                                                                                                                BIHARAMULO.
KUMB.Na.ED/NSS/S1349/V0L2/2016                                                                       ………… ……………………………
Blog: nyakahuras1349.blogspot.com 
Ndugu………………………….…………………………..
…………………….…………………………………………….



FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO- 2016.   KWA MASOMO YA ……………….

  1. Ninayofuraha kukufahamisha kuwa umechaguliwa kuingia kidato cha tano katika shule hii mwaka 2016 .

Shule ya Sekondari  Nyakahura ipo Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, umbali wa kilometa 75 magharibi ya makao makuu ya wilaya ya Biharamulo.

Muhula wa kwanza wa masomo unaanza tarehe ………………unatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe…………………..na mwisho wa kuripoti ni tarehe………………………..
          Mambo muhimu ya kuzingatia.
     2            SARE ZA SHULE
    1. WASICHANA
  - DARASANI
(i)               Sketi nyeusi mshono wa rinda bokisi au suruari kwa wasichana wa kiislamu (Hijjabu)
(ii)            Shati mbili nyeupe za mikono mirefu aina ya Tetron.
(iii)       Viatu vya ngozi nyeusi jozi mbili visivyo na kisigino kirefu.
(iv)            Soksi ndefu nyeupe zisizo na maandishi ya aina yoyote.
(v)            Sweta kwa ajili ya baridi (inapatikana shuleni 14,000/=)
Hijjabu kwa wasichana wa Kiislamu kwa wale watakaopenda kuvaa hivyo. Rangi ya Hijjab ifanane na sare ya shule.
                     -NJE YA DARASA
(i)   Gauni  rangi ya damu ya mzee (maruni) kitambaa cha sukarisukari vilevile  shuleni  

    1. WAVULANA
-DARASANI
(i)          Suruwali nyeusi   (yenye marinda mawili kila upande)
(ii)           Shati mbili nyeupe za mikono mirefu
(iii)           Viatu vya ngozi nyeusi jozi mbili.
(iv)          Soksi nyeusi
(v)            Sweta kwa ajili ya baridi (inapatikana shule Tshs.14,000/=)
-NJE YA DARASA
            (i)  Suruali ya kushindia kitambaa rangi ya damu ya mzee (maruni)

NB: Vitambaa vya sare ya shule vinapatikana shuleni

Ada na michango ya shule:-
(a). Ada ya shule kwa mwaka ni shilingi 70,000/=, unatakiwa kulipa shilingi 35,000/= kwa        muhula mmoja.
(b). Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni:-                                                                                                                        
(i)   Tsh 20,000/= ukarabati
         (ii)   Tshs 20,000/= kwa ajili ya tahadhari
         (iii)  Tshs 15,000/= kwa ajili ya kutengeneza kiti na meza
(iv) Tshs 15,000/= kwa ajili ya taaluma
(v)  Tshs 5,000/= kwa ajili ya walinzi
     (vi) Tshs 5,000/= kwa ajili ya wapishi
         (vii   Tshs 50,000/=   kwa ajili ya kutengeneza Kitanda kwa sababu vilivyopo havitoshi.
         (viii) Tshs 30,000 Matibabu
                        Jumla kuu   230,000/=
                    Michango hiyo ilipwe kwenye akaunt hii NYAKAHURA SEC SCHOOL RECURRENT 3171200096.(NMB)
NB. KILA MWANAFUNZI AJE NA BANK PAYS SLIP INAYOONYESHA MICHANGO HIYO.

            B)
        (i)      Tshs 5,000/= kwa ajili ya kitambulisho
        (ii)     Tshs  14,000/= Sweta
            (vi)    Tshs  4000/=   picha za passport size.
       (v)     Tsh 12,000/= mchango wa tsherti. (ya kora)
          (vi)    Tsh 5000 /= kwa ajili ya tai   
                  Jumla kuu  40,000/=
              Michango hiyo aje nayo shuleni, asiweke kwenye account ya shule

  Vifaa vya malazi, chakula na usafi:-
(i)                               Reki na  mopa kwa wasichana  
(ii)                             Mifagio ya ndani na nje ( soft broom na hard broom) ya plastic kwa wavulana 
(iii)                            Godoro la  ft 21/2 ,Sahani,  Bakuri, kikombe na kijiko kwa ajili ya chakula
(iv)                            Ndoo moja  ya plastic lita 20  ya matumizi  ya shule pia mwanafunzi anashauriwa kuja na ndoo ya matumizi yake binafsi pamoja na beseni.
(v)                             Mwanafunzi lazima aje na Chandarua
(vi)                            Blanketi - Ni muhimu kuja nayo.
(vii)                          Shuka mbili za rangi ya pinki.
(viii)                         Rim A4
(ix)                            Toilet paper – 10 (mhula wa kwanza 5)
N.B    ili kuepuka usumbufu wa kubeba mizigo baadhi ya vifaa vinapatikana  katika maduka yaliyopo  jirani na shuleni ni pamoja na;   Reki, mopa, soft bloom, hard bloom,           ndoo, godoro, sahani, bakuli, kikombe, kijiko, beseni, chandarua, toilet paper, rim, daftari,shuka, shati za shule na mathematical set   
Vifaa vya masomo:-
(i)                               Daftari 5 kubwa kwa kuanzia (Counter book)
(ii)                             Daftari 10 ndogo kwa ajili ya majaribio ya mwezi.
(iii)                            Kalamu ya wino-bluu au nyeusi
(iv)                            Mfuko wa vitabu (school bag).
(v)                             Mathematical set
(vi)                            Dictionary
(vii)                          Mwanafunzi  aje na kitabu kimojawapo katika masomo ambayo amechaguliwa

Vifaa vya michezo
Utatakiwa kuwa na vifaa vya michezo vifuatavyo, ili kuvitumia wakati wa michezo mbalimbali hapa shuleni na nje ya shule.
(i)                               Viatu vya raba
(ii)                             Bukta mbili  kwa wavulana rangi ya bluu.  
(iii)                            Track kwa wasichana rangi ya bluu.
(iv)                            Fulana (T-shirt) rangi ya bluu.

Sheria na kanuni muhimu za shule hii:-
Shule inaendeshwa, kwa mujibu wa sheria ya elimu Na 25 ya mwaka 1978. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na wizara yenye dhamana ya elimu nchini. Pamoja na fomu hii ya kujiunga na shule, naambatanisha sheria  za shule hii.

Mahitaji mengine:-

a.        Afya ya mwanafunzi. Nimeambatanisha “Medical examination form” ambayo itajazwa na mganga Mkuu wa Hospitali ya serikari.  Fomu hii itakabidhiwa kwa mkuu wa shule mara utakaporipoti shuleni.
NB.  
Uongozi wa shule unakutakia maandalizi mema na safari njema ya kuja hapa shuleni.
NAZIDI KUWAKUMBUSHA  KUWA MKIWEKA MICHANGO HIYO KWENYE BENK ANDIKA NA JINA LA ALIYETUMA FEDHA HIZO.
               NACHUKUA NAFASI HII TENA KUKUPONGEZA NA KUKUKARIBISHA .
                    Wako katika Ujenzi wa Taifa

                 BOAZ P. KAMUGISHA (MAKAMU WA MKUU WA SHULE)
                             SIM. 0766235699/ 0786087767


                    R.ISHENGOMA (MKUU WA SHULE)
                     SIMU 0752134334/ 0787201405
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SEKONDARI NYAKAHURA

SHERIA NA KANUNI ZA SHULE
Sheria za shule zinatungwa kufuatana na maadili ya Taifa letu. Lengo ni kutoa mwongozo na msaada kwa mwanafunzi ambaye anatarajia awe raia na mzalendo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Utii wa sheria za shule ni utii wa sheria za Taifa letu.  Shule imepewa jukumu la kulea na kuelimisha vijana ili badaye wawe raia wema wa Taifa hili. Sharti mwanafunzi kufuata kanuni na sheria za shule.

Zifutazo ni sheria za shule na kila mwanafunzi anatakiwa aziheshimu na kuzizingatia ipasavyo:-
  1. Mwanafunzi sharti aweheshimu walimu na wafanyakazi wote wa shule ambao ni walezi wake. Ajiepushe na lugha chafu, utovu wa nidhamu kwa walezi hawa. Inampasa mwanafunzi kusimama sawa anapomwona mwalimu au mfanyakazi na mgeni na yeyote yule ambaye anamzidi umri na kumuamkia ipasavyo.
  2. Ni kosa kubwa kwa mwanafunzi kukataa kufanya kazi za shule, au adhabu ya mwalimu au kiongozi yoyote yule wa wanafunzi aliye chaguliwa kwa mujibu wa sheria.
  3. Kila mwanafunzi ni lazima ahudhurie vipindi vyote vya darasani na nje alivyopangiwa kwa wakati uliopangwa. Ni kosa kubwa kukosa vipindi bila sababu maalum.
  4. Nimarufuku mwanafunzi kutoka nje ya mipaka ya shule isipokuwa kwa kibali maalumu cha mkuu wa shule. Kila mwanafunzi atawajibika kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia kikamilifu maelezo juu ya kuwepo ndani na nje ya mipaka ya shule wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii.
  5. Kila mwanafunzi atalazimika kuzingatia ratiba ya siku nzima na kuitekeleza ”Daily Routine”
  6. Kila mwanafunzi analazimika kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa shule na nje ya shule.
  7. Kila mwanafunzi analazimika kuhudhuria maandalio ya jioni (Night Preparation)
  8. Ni lazima mwanafunzi ajiepushe na makosa ambayo yanaweza kusababisha afukuzwe shule.

Ø  Wizi
Ø  Uasherati, ubakaji na ushoga.
Ø  Ulevi na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
Ø  Uvutaji wa bangi.
Ø  Makosa ya jinai
Ø  Kupigana au kupiga
Ø  Kuharibu kwa makusudi mali ya umma
Ø  Kudharau Bedera ya Taifa na picha za viongozi wakuu wa serikali.
Ø  Kuoa au kuolewa.
Ø  Kupata mimba au kusababisha mimba  ndani na nje ya shule.
Ø  Kutoa mimba.
Ø  Kugoma, kuchochea na kuongoza au kuvuruga amani na usalama wa watu.
Ø  Kukataa adhabu makusudi.
Ø  Kuwa na simu ya mkononi
Ø  Kuvaa suruwali aina ya modal shuleni

  1. Wanafunzi hawaruhusiwi kutembelea sehemu zifuatazo isipokuwa kwa kibali maalumu:-
Ø  Chumba cha walimu (staff room)
Ø  Ofisi za shule
Ø  Maabara
Ø  Jikoni
Ø  Nyumba za walimu na wafanyakazi wasio walimu

10.    Ni marufuku kwa mwanafunzi kutembelea sehemu zifuatazo:-
Ø  Vilabu vya pombe
Ø  Majumba ya sitarehe
Ø  Majumba ya kufikia wageni.
11.           Ni marufuku wanafunzi kuvaa kofia, viatu vya ghorofa na mapambo mengine mfano herein, vidani, mikufu na bangili Nk.
12.       Ni wajibu wa kila mwanafunzi kufanya usafi wa mazingira pamoja na usafi wake binafsi. Nywele ndefu haziruhusiwi; hivyo ni wajibu wa kila mwanafunzi kuhakikisha nywele zake ni fupi.
13.        Ni kosa mwanafunzi kutumia lugha mbaya kwa wanafunzi wenzake, kwa mwalimu au kwa watu wengine. 
14.        Mwanafunzi haruhusiwi kumiliki simu ya aina yoyote ile awapo hapa shuleni.
    15    Kila mwanafunzi lazima aje na cheti cha kuzaliwa na cheti kinachothibitisha afya yake kutoka
      katika Hospitari ya serikali ya Wilaya ,Mkoa au Teule.
 
SKETI: IVUKE  MAGOTI NA ISHONWE KAMA INAVYOONESHWA KATIKA MCHORO HUU

NB: 
SURUALI NI SHARTI IWE NA RINDA MBILI KILA UPANDE NA CHINI MIGUUNI IWE IMEFUNGWA

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA  NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SEKONDARI - NYAKAHURA

FOMU YA KUANDIKISHWA–SHULE
(Ijazwe kwa herufi kubwa na irejeshwe kwa mkuu wa shule)

  1. Jina kamili……………………………………………………………………………………..

Tarehe ya kuzaliwa………………… Wilaya…………………..Mkoa……….………
Taifa………...Dini:RC/Anglican/Lutheran/Muslim/Pentecoste/n.k…………..
Shule ya sekondari unayotoka…………………………………………………….…...

2.       Jina la Baba/Mama/Mlezi……………………………………………………………..….
Anwani yake………………………………………………………………………………….
Kazi ya Baba/Mama/Mlezi………………………………………………………………..
Namba ya simu…………………………………………………..………………………….

  1.  
AHADI YA MWANAFUNZI.
(a)     Mimi………………………………….nimeyasoma na kuyaelewa maelekezo yote ambayo ni pamoja na sheria na kanuni za shule na nimekubali kuingia kidato cha tano katika shule ya sekondari Nyakahura kuanzia tarehe…………………..hadi nitakapo maliza kidato cha sita.
(b)     Kwa hiyo naahidi kwamba:-
(i)                               Nitazitii sheria zote za shule na kutimiza mambo yote muhimu yaliyotajwa
(ii)                             Sitashiriki vitendo vya hujuma wala vitendo ambavyo vitakuwa kinyume na uongozi wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
(iii)                            Nitatunza mali ya umma ambayo ni pamoja na majengo, samani, vitabu n.k.

Tarehe …………………sahihi ya mwanafunzi……………………………………..


AHADI YA MZAZI/MLEZI.

Mimi …………………………………………………..…………….ambye ni mzazi/mlezi wa mwanafunzi……………………………………………………………….ninahaidi kwamba:-

  1. Nitashirikiana na uongozi wa shule, walimu na watumishi wasio walimu katika kuhakikisha, mwanangu anatii sheria na kanuni za shule ya sekondari Nyakahura na iwapo atashindwa kutii sheria hizo, nitalazimika  kumuondoa katika hosteli.

2. Nitafanya kila niwezalo kumwezesha mwanangu, kusoma kwa kulipa Ada na michango mingine kama ilivyoelekezwa na shule.

     Tarehe…………………………………………………………………………………………
Sahihi………………………………………….Namba ya simu:…………



No comments:

Post a Comment